Kilimanjaro Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya katika Uwanja wa Ufundi mjini Jinja.

Wafungaji wa magoli ya Kilimanjaro Queens  ni Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Stumai Abdallah dhidi ya moja la Kenya, lililofungwa na Christine Nafula.

Kilimanjaro Queens iliingia fainali baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Uganda, wakati Kenya iliifunga 3-2 Ethiopia.

Kilimanjaro Queens iliongoza Kundi B baada ya kushinda kura ya sarafu kufuatia sare ya 0-0 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, hivyo kufungana nayo kwa pointi na wasatani wa mabao kileleni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *