Timu ya taifa ya wanawake Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Queens’ imetinga fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Uganda.

Kilimanjaro Queens itakutana na Kenya, ambayo imeifunga 3-2 Ethiopia katika nusu fainali iliyofanyika jana.

Mabao ya Tanzania Bara yamefungwa na Donosia Daniel dakika ya sita, Mwanahamisi Omari dakika ya 17, Stumai Abdallah dakika ya 31 na Asha Rashid.

Fainali ya CECAFA Challenge ya kwanza ya wanawake inatarajiwa kufanyika Septemba 20, ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Tovuti hii inawatakiwa kila la kheri Kilamanjaro Queens kwenye fainali hiyo itakayofanyika kesho nchini Uganda.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *