Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ya wanawake ‘Kilimanjaro Queens’  imefuzu Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rwanda.

Kwa kuwa Kundi B lina timu tatu, nyingine Ethiopia, ushindi unaihakikishia Kili Queens tiketi ya Nusu Fainali.

Mabao ya Kili Queens yamefungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya Rwanda yamefungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.

Kili Queens watashuka tena dimbani kumenyana na Ethiopia Septemba 16, mwaka huu katika mchezo wa mwisho wa kundi lake. Rwanda na Ethiopia zitakamilisha mechi za Kundi B kwa kumenyanaa na Septemba 14.

Nusu Fainali zitafuatia Septemba 18 kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *