Mwanamuziki nyota wa Marekani, Beyonce Knowles ameshindwa kutumbuiza kwenye sherehe za utoaji wa tuzo za Emmy baada ya kusumbuliwa kiafya na kumfanya ashindwe kuhudhuria sherehe hizo.

Mwanamuziki huyo alitakiwa kutoa suprise perfomance usiku wa tuzo hizo lakini ilishindana kutokana na afya yake kudorora kipindi cha sherehe hizo.

Emmy Awards ni tuzo zinazotolewa kwa mastaa wa filamu kila mwaka ambazo zimefanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater, Downtown katika mji wa Los Angeles nchini Marekani Marekani.

Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilifanyika usiku wa Sepetemba 18 mwaka huu ambapo jumla ya tuzo 68 zilitolewa usiku huo huku filamu ya ‘The Game of Thrones kuibuka kidedea kwenye tuzo hizo baada ya kunyakua tuzo 10.

Beyonce ni miongoni mwa wanamuziki maarufu duniani ambapo ameanza muziki kitambo lakini mpaka sasa bado anaendelea kutamba kutokana na ngoma zake kuwabamba mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *