Kilango: Kuteuliwa kwangu kumetokana na uwezo nilionao

0
282

Baada ya kuteuliwa ubunge wa viti maalu na Rais Magufuli, Anne Kilango Malecela amesema uteuzi wake umetokana na uwezo na uzoefu alionao katika uongozi.

Mbunge huyo mteule aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dk. John Magufuli mapema mwaka jana kutokana na kushindwa kubainisha watumishi hewa.

Pia Kilango amesema anamshukuru Rais Magufuli kwa kutambua uwezo wake wa kuchapa kazi huku akiahidi kuendelea kuwatetea wananchi wa Same Mashariki na Watanzania kwa ujumla.

Vile vile amesema atafanya kazi kwa moyo wote kuwakilisha Tanzania na chama chake bila ubaguzi wowote.

Kilango aliteuliwa juzi usiku na Rais Dk. Magufuli. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa mbunge huyo ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

LEAVE A REPLY