Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Edward Lowass katika mazishi ya aliyekuwaya mfanyabiashara maarufu, Faustin Mrema yaliyofanyika Ngurudoto mkoani humo jana.

Maelfu ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa madhehebu mbalimbali wa dini, wafanyabiashara wakubwa katika sekta ya utalii, wanasiasa, viongozi wastaafu ni miongoni waombelezaji waliomsindikiza tajiri huyo aliyeaga dunia akipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini hivi karibuni.

 Mwili wake umepumzishwa katika eneo jipya la makaburi ya familia jirani na hoteli yake ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge iliyopo Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Katika mazishi hayo, Lowassa alimzungumzia marehemu kama mtu atakayekumbukwa kwa matendo yake ya kuwajali watu wanyonge.

Kikwete ambaye hakuzungumza chochote alikua kivutio kwa viongozi na wananchi waliotaka kumsalimia lakini umati wa watu na ulinzi ndiyo vilikuwa vikwazo kwa wananchi huku muda wote akiwa katika hali ya maombolezo

Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni waziri wa zamani wa mambo ya nje, Bernard Membe, waziri wa zamani wa fedha, Baziri Mramba, wabunge na wakuu wa wilaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *