Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema muda si mrefu Tanzania itaandikwa na wino wa dhahabu kwenye sekta ya michezo.

Kikwete aliyasema hayo jana katika fainali za michuano ya mpira wa kikapu kwa vijana zilizofanyika kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.

Kikwete amesema kuwa “Kituo hiki kwa sasa kina vijana 50,000 wanaojiendeleza kwa soka na mpira wa kikapu, wachezaji wawili wamechaguliwa timu ya soka ya taifa,”.

Aidha Rais Kikwete alisema katika uongozi wake amejitahidi kuhakikisha michezo inakua kwa kutengeneza mazingira bora kwa kuwalipa walimu wa kigeni wa timu za taifa.

Akizungumzia fainali hizo ambazo timu ya shule ya msingi ya Lord Baden iliifunga Tusiime vikapu 22-18, Kikwete alisema michuano hiyo ya vijana itazalisha wachezaji bora kama Alana Benard wa Marekani ambaye yupo nchini kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *