Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kupitia kikosi chake cha Usalama Barabarani kimekusanya zaidi ya Sh milioni 690, kupitia tozo za makosa ya usalama barabarani.

Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro amesema faini hizo ni kuanzia Oktoba 18 hadi 25 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Sirro idadi ya magari yaliyokamatwa yalikuwa ni 20,833, idadi ya pikipiki zilizokamatwa zilikuwa ni 2,171 na daladala zilizokamatwa zilikuwa ni 8,435.

Alisema magari mengine ambayo ni binafsi na malori yaliyokamatwa yalikuwa ni 12,398 na waendesha bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmeti na kupakia mshikaki walikuwa 96.

Kamanda Sirro amesema jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 23,004 na fedha zilizotozwa ni 690,120,000 na hivyo kuiingizia serikali mapato.

Pia ametoa wito kwa wananchi wote kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuondokana na ajali zisizo za lazima zinazosababisha majeruhi na wakati mwingine vifo kwa watu wasio na hatia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *