Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kimefanya mazoezi katika kambi ya kijeshi kwa ajili ya kujifunza uzalendo wa nchi hiyo.

Timu hiyo imefanya mazoezi kwa masaa 48 kwa ajili ya kujiweka fiti na kujifunza uzalendo wa nchi hiyo wanapokuwa katika mashindano tofauti.

Wachezaji wa Uingereza wakiwa wamevalia sare za kijeshi ndani ya kambi hiyo.
Wachezaji wa Uingereza wakiwa wamevalia sare za kijeshi ndani ya kambi hiyo.

Kikosi hicho ambacho kinatarajia kucheza mechi yake ya kufuzu kucheza kombe la dunia dhidi ya Scotland kimefanya mazoezi tofauti ndani ya kambi ya hiyo ambapo wachezaji wote walivalia sare za kijeshi.

Wachezaji hao walionekana kufurahia mazoezi hayo kutokana na kila mmoja kushiriki mazoezi hayo kwa bidii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *