Kikosi cha timu ya Bunge la Tanzania kilichosheheni wachezaji wa michezo ya mpira wa miguu,wavu, riadhaa, kuvuta kamba na mchezo wa gofu chenye wachezaji 60 kimeingia kambini mkoani Tanga.

Mwenyekiti wa timu ya Bunge, William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza amesema kuwa maandalizi kwa upande wa timu yao yamekamilika kwa asilimia kubwa.

Amesema kutokana na umuhimu wa mashindano hayo waliamua kuweka kambi mkoani Tanga ili kuendana na hali ya hewa kabla ya kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mpango wa kuimarisha kikosi chao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la timu ya Bunge, Stephen Ngony’ani maarufu kama Proffesa Maji Marefu amesema kuwa kikosi chao kimejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Pia amesema timu hiyo ipo kwenye mazingira mazuri ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mashindano hayo ili kuweza kutimiza dhamira yao waliojiwekea ya kutwaa ubingwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *