Klabu ya Simba imetangaza kikosi chake kitakacho shuka uwanjani hii leo kuwakabili Tanzania Prisons.

Kwenye kikosi hicho cha Simba SC wachezaji watakao anza ni, John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe, Mkude, Zimbwe JR, Asante Kwasi, Mlipili, Juuko, Nyoni na Aishi Manula.

Kikosi cha akiba wapo, Nduda, Mavugo, Kotei, Mzamiru, Paul Bukaba, Gyan na mchezaji mwingine ni Rashid.

Simba SC inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na jumla ya pointi 55 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na hasimu wake Yanga SC yenye alama 47 huku Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwa kuwa na 46.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *