Kijana Baraka Elias ambaye ni mrefu mwenye futi saba anayesumbuliwa na ugonjwa wa nyonga anatarajia kwenda kutibiwa nje baada ya jopo la madaktari kufikia uamuzi huo kutokana na ukosefu wa vifaa.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia gharama kubwa za kuagiza kifaa pandikizi (implant) kutoka nje ya nchi ambacho angewekewa kubadilisha nyonga yake iliyovunjika.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MOI, Almas Jumaa amesema Baraka atakwenda kutibiwa nchini India.

Amesema MOI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa pamoja wamekubaliana Baraka aende kutibiwa nje ili kupunguza mzigo wa gharama.

Awali ilielezwa kuwa MOI ilishindwa kumfanyia upasuaji kijana huyo kutokana na urefu aliokuwa nao kutoakana na mashine za MOI haziendani na urefu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *