Mkurugenzi wa mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila ameendelea kusota rumande mpaka sasa huku dhamna yake ikiwa bado haijatolewa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa, amethibitisha kuwepo kwa Kigaila rumande katika kituo kikuu cha polisi kanda maalum, na kusema kwamba bado wanamshikilia Kigaila mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na kumpa dhamana, na hatimaye kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

“Kigaila bado tunaye dhamana yake bado hajapata, tunaendelea na uchunguzi tukijiridhisha tutampa dhamna na kumpeleka mahakamani kujibu mashtaka yake”.

Kigaila alienda kuripoti jana kituoni kufuatia wito aliopewa na jeshi la polisi jijini Dar es salaam, na kuwekwa rumande mpaka sasa mbako yupo kutokana na tuhumza za kutoa uchochezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *