Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Francis Kifukwe amemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji anayetaka kuikodisha klabu kwa miaka 10 kuwasilisha mapendekezo yake kwa maandishi.

Kifukwe amesema kwamba baada ya Mkutano wa Jumamosi, alimuambia mwenyekiti huyo awasilishe maombi yake kwa maandishi.

Wanachama wa Yanga kukubali kubadilisha mfumo wa kuiendesha klabu huyo na kuafiki kuimilikisha kwa mtu mmoja, lakini watalazimika kusubiri taratibu zifuatwe.

Katika mkutano mkuu wa dharula uliofanyika Jumamosi ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, wanachama wa Yanga walikubali kumkodisha klabu Mwenyekiti wao kwa miaka 10.

Hiyo ilifuatia Manji kutoa pendekezo la kukodisha klabu kwa miaka 10 amilikishwe nembo na timu na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *