Wahifadhi wa eneo la Sasakwa Singita Grumet wamesema kuwa hakuna kaburi la ‘Faru John’ kwa kuwa hakuzikwa.

Hayo yanafuatia baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutangaza kuunda timu mpya kuchunguza mazingira ya kifo cha faru huyo huku akihoji mambo manne yaliyozua utata.

Mambo manne aliyoyahoji waziri mkuu kuhusu kifo cha Faru John ni aliumwa lini, aliumwa nini, daktari gani aliyemtibu na zilipo taarifa za matibabu yake.

Pia Waziri mkuu aliagiza mwili wa faru huyo kufukuliwa na kutazama kama vinasaba vyake vinaendana na watoto wake 26 ambao bado wapo katika Creta ya Ngorongoro mkoni Arusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *