Mwanamuziki nyota wa Marekani, Lil Wayne amekimbizwa hospitali baada ya kuanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa unaomsumbua.

Lil Wayne ambaye siku ya jana alikuwa na tamasha lake katika ukumbi wa Drais Beachclub mjini Vegas, lilikatishwa  baada ya msanii huyo kukutwa akiwa hana fahamu  na ikaelezwa kuwa ameanguka kutokana na ugonjwa wa kifafa.

Kwa mujibu wa vyanzo viwili vya karibu zimeeleza kuwa rapper huyo amelaza  katika hospitali ya Northwestern Memorial iliyopo mjini Chicago, baada ya kukutwa amepoteza fahamu katika chumba cha hotel cha Westin- Michigan Avenue.

Naye Daktari aliyekuwa akimtibua msanii huyo amemtaka apumzike kwa siku kadhaa ili afya yake iweze kurudi katika hali ya kawaida licha ya kuwa aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo siku ya jana.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii huyo kuugua na kuanguka kutokana na ugonjwa huo wa kifafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *