Muigizaji na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo A.K.A Kidoti ameanzisha mpango maalum wa kufundisha somo la ujasiliamali kwa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Majani ya Chai iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kidoti ataanza kutoka mafunzo hayo kwa wanafunzi wa kike katika shule hiyo kuanzia wiki ijayo kwa lengo la kuwapa ufahamu wanafunzi hao na kuweza kuanzisha biashara zao baada ya kumaliza elimu ya Sekondari.

jokate-1

Mrembo huyo amesema kuwa mafunzo ya ujasiliamali kwa wanafunzi ni muhimu sana kutokana na kuweza kujipanga kwa wanafunzi kukabiliana na maisha baada ya kuhitimu elimu yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Jokate ameongeza kwa kusema kuwa elimu ya ujasiliamali inaweza kumkomboa mtu kutokana na tatizo la uhaba wa ajira uliopo sasa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *