Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani imetangaza nafasi 45 za ajira kwa wanaotaka kuwa watendaji wa vijiji wilayani humo.

Imesema imetangaza ajira hizo, ili kupata watendaji wa vijiji watakaoziba mapengo ya waliofariki na walioachishwa kazi kutokana na kuwa na elimu ya darasa la saba.

Kibiti ni miongoni mwa wilaya za mkoa wa Pwani ambazo kwa miaka miwili iliyopita, zimekumbwa na mauaji ya viongozi wa ngazi mbalimbali, wakiwamo watendaji na wenyeviti wa vijiji.

Mauaji hayo yalikuwa yakitekelezwa na watu wasiofahamika, waliokuwa wakivamia nyumba za watendaji hao na kuwaua kwa kuwapiga risasi.

Wilaya nyingine za mkoa huo zilizokumbwa na mauaji hayo ni Rufiji na Mkuranga.

Aidha, kutokana na kushamiri kwa mauaji hayo na vitisho vilivyokuwa vikitolewa na wauaji, baadhi ya watendaji wa vijiji waliripotiwa kukimbia makazi yao wakihofu kuuawa.

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoye, alisema hali ya wilaya yake kwa sasa ni shwari.

Kutokana na kurejea kwa hali ya utulivu wilayani humo, Ndabagoye alisema wameona sasa kuna haja ya kutangaza nafasi za kazi 45 za watendaji wa vijiji.

Ushwari huo unatokana na juhudi za Jeshi la Polisi, mkuu wake Inspekta Generali (IGP) Simon Sirro, ambaye baada ya kuteuliwa amefanikiwa kukomesha mauaji hayo huku jeshi hilo likitangaza kuwaua watuhumiwa 13 wa mauaji hayo kwa mpigo katika shambulizi moja, na wengine kukimbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *