Mkali wa Bongo fleva, Alikiba amewasili Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki hafla ya utoaji tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika kesho.

Katika safari yake hiyo Alikiba ameongezana na kiongozi wake wa Rockstar4000, Seven Mosha na meneja wake Aidan pamoja na mwanamuziki mwenzake Barakah The Prince.

Alikiba ni miongoni kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo kesho katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mwanamuziki huyo pia anawania tuzo ya β€˜Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae alioshirikiana na Sauti Sol kutoka Kenya.

Kwa upande wa Tanzania ukiacha Alikiba wasanii wengine watakaoshiriki tuzo hizo ni mpinzani wake Diamond Platnumz, Rayvanny pamoja na kundi la Navy Kenzo lenye wasanii wawili Aika na Nahreel.

MTV MAMA ni tuzo kubwa barani Afrika ambazo zinafanyika kila mwaka na kushirikisha wasanii mbali mbali kutoka bara la Afrika pamoja na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *