Mwanamuziki mkongwe wa taarabu nchini, Khadija Yusuph amesema kwamba kundi la Jahazi Morden Taarabu kwa sasa limevunjika na tayari wamegawana vitu vilivyokuwa ndani ya kundi hilo na yeye kwa sasa yupo kwa Thabit Abdul.

Khadija amesema Jahazi limevunjwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa Mzee Yusuph wakati anaacha muziki alisema hata vunja kundi hilo lakini Mungu mwenyewe ndo atalivyunja na tayari dua yake imepokelewa na Mungu.

Pia Khadija amesema kwa sasa furaha ya kaka yake Mzee Yusuph imekamilika kwa sasa na dua zake pia zitakuwa  zimepokelewa na Mungu kama alivyokuwa akiomba kwamba ifikie kipindi hata nyimbo zake zisiwe zinapigwa.

Kundi la Jahazi ni kundi lililojizolea umaarufu nchini kupitia nyimbo zao mbali mbali kwasasa limekufa baada ya mzee Yusuf kuacha kuimba na kumrudia mungu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *