Mwanamuziki wa taarabu nchini, Khadija Yusuph amemshauri wifi yake Leila Rashid kufuata nyayo za mumewe na kuachana na maswala ya muziki.

Khadija amesema kuwa Reila anatakiwa kumfuta mume wake Mzee Yusuph kwa kuwa tayari mume wake kashaenda hija na ni dhambi kuacha kumsikiliza mume wake.

Khadija amesema ni vizuri Leila kumfuata mume wake kwa kuwa haoni sababu ya yeye kuendelea kuwa na kundi la Jahazi wakati mume wake Mzee Yusuph ameamua kumrudia Mungu na kuachana na maswala ya muziki.

Vile vile Khadija Yusuph amewaambia mashabiki waendelee kusubiria maamuzi ya Mzee Yusuph mwenyewe juu ya maamuzi ya mke wake kuendelea na muziki wakati yeye kaamua kumrudia Mungu na kuachana kabisa na mambo ya dunia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *