Makundi ya muziki wa taarab nchini TOT pamoja na Africa Taarab leo yanatarajia kutoa burudani kwenye siku ya wapendanao ‘Valentine Day’ katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Meneja wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema kuwa nyimbo nyingi zitaolewa kwenye  usiku huo ulioandaliwa kwa ajili ya wapendao.

Pia Mbizo amesema kuwa kapo 100 wa kwanza watakaopendeza watapata sapraizi kibao ambazo zimeandaliwa na ukumbi huo sambamba na huduma bora ya VIP.

Malkia wa mipasho nchini Khadija Kopa ambaye anatarajia kuongoza kundi zima la TOT Taarab amewataka mashabiki wake wajitokeze kwa wingi usiku wa leo Dar Live kwani amepania kuwaonyesha mashabiki wake Taarab ilivyo.

Kwa upande wake Mwanahawa Ali ambaye ataongoza kundi la Africa Taarab amesema hatawaangusha mashabiki wake kwani wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kutoa burudani.

Burudani hiyo itakuwa kwa ajili ya siku ya Wapendanao ‘Valentine Day’ ambayo itafanyika leo duniani kote kudumisha upendo kwa wapendanao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *