Comedian  maarufu nchini Marekani, Kevin Hart amepata tuzo ya heshima ya Hollywood ijulikanayo kama Hollywood Walk of Fame kutokana na mchango wake katika suala zima la sanaa.

Kupitia ukarasa wake wa Instagram Kevin Hart ameandika ‘Uwezi kufanya vitu peke yako…..unatakiwa kuwa na timu inayokuamini kwa muono wako’.

Mastaa wengine waliowahi kupatiwa heshima kama hiyo ni pamoja na Shirley Caesar, Clarence Avant, Michael Jackson, Paula Abdul, Madonna, Beyonce, Celine Dion pamoja na Usher Raymond.

Kevin Hart  ndiye mchekeshaji anayeongoza kulipwa fedha nyingi kuanzia mwezi Juni mwaka jana akiwa ameingiza kiasi cha $87.5 milioni kulingana na jarida la Forbes.

Hollywood Walk of Fame ni tuzo ya heshima inayotolewa kwa mastaa wa Marekani kulingana na mchango wao katika jamii pamoja na na kazi yake anayoifanya katika kazi ya sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *