Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imeshindwa kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa,  mwendesha mashtaka wa serikali aliiambia mahakama kwamba shahidi wa jamhuri aliyepaswa kuwasilisha ushahidi wake leo dhidi ya mbunge huyo ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema, amepata dharura ya kikazi.

Kutokana na kuridhishwa na maelezo hayo, hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo ambayo inatarajiwa kusikilizwa tena, Februari 14.

Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Juni 28, 2016.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *