Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itaendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Juni 8 huu katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa TBC, Tido Mhando.

Wakili wa Takukuru, Leonard Swai jana amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa  kesi  inayomkabili Tido leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa  mashahidi wa upande wa mashtaka.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameiahirisha kesi hiyo hadi Juni 8 ili mashahidi wa upande wa mashtaka waendelee kutoa ushahidi.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri wamekwishatoa ushahidi .

Mashahidi hao ni  Ofisa uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *