Kesi inayomkabili Salum Njwete (34) maarufu kama ‘Scorpion’ inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 30 mwaka huu baada ya upelelezi kukamilika.

Hayo yamesemwa na hakimu Flora Lymo anayesikiliza kesi hiyo ya unyang’anyi inayomkabili Scorpion.

Kwa upande wake Scorpion aliomba asomewe maelezo ya awali lakini hakimu alikataa kufanya hivyo.

Scorpion anakabili na kesi ya kumtoboa macho, kumjeruhi tumboni na kumpora fedha na mkufu Said Mrisho maeneo ya Buguruni Sheli jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *