Kesi ya mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Ndama Shaaban Hussein almaarufu Pedeshee Ndama Mutoto ya Ng’ombe leo  imeahirishwa tena kutokana na upelelezi kutokamilika.

Keis hiyo imeghairishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa kosa la utapeli wa dola za Kimarekani 540, 390 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1.

Ndama awali kesi yake ilipopanda Kisutu alisomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu, Victoria Nongwa na Mwendesha Mashtaka Leonard Msigwa akisaidiana na Christopher Challo kuwa, mnamo Februari 20, 2014 mkoani Dar, Ndama alitengeneza nyaraka feki, zikionesha kupata kibali cha kusafirisha sampuli za madini ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Shtaka la pili, tatu na nne pia yalikuwa ya kugushi nyaraka, ikiwemo iliyotoka Umoja wa Mataifa, iliyoisafisha kampuni yake ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Ltd kuwa imeruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu.

Nyaraka hizo zililenga kuiaminisha Kampuni ya Trade TJL DTYL Ltd ya Australia kuwa Muru ni watu halali kwa biashara hiyo. Pia Ndama alidaiwa kugushi nyaraka zilizoonesha kuwa alilipa kiasi cha dola 331, 200 sawa na shilingi milioni 728 kwa TRA kama kodi ya kupitisha mzigo huo hapa nchini.

Shtaka la tano la Ndama ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kiasi cha dola 540,390 kutoka kampuni hiyo ya Australia zilizowekwa katika akaunti ya Kampuni ya Muru katika Benki ya Stanbic na shtaka la sita lilihusu kosa la utakatishaji fedha hizo.

Ndama alikana mashtaka yote na kesi yake ikaahirishwa hadi Desemba 13, ambapo leo tena imeahirishwa hadi Desemba 27 mwaka huu itakapotajwa tena.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *