Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeghairisha kesi inayomkabili mtuhumiwa wa makosa ya kukamatwa na nyara za serikali, Yusuf Ali Yusuf maarufu kama Shehe Mpemba (35) hadi Desemba 15 kufuatia kutokukamilika kwa upelezi wa kesi hiyo.

Wakili wa Serikali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Thomas Simba amewasilisha hoja kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo Hakimu Simba aliamua kuipanga kesi hiyo isikilizwe tena Desemba 15 mwaka huu na kumtaka wakili huyo akamilishe haraka upelelezi ili kesi hiyo isikilizwe na kutolewa maamuzi.

Mpemba na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kula njama za kufanya uhalifu na kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria.

Mtuhumiwa huyo na wenzake Charles Mrutu (37), Benedict Kungwa (40), Jumanne Chima (30), Ahmed Nyagongo (33) na Pius Kulagwa (46)  hawakutakiwa kujibu chochote na kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba Mosi (leo), na watuhumiwa hao walirudishwa rumande.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *