Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imehairishwa Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media, Maxence Melo iliyokuwa isikilizwe leo Januari 16, 2017.

Wakili wa Jamhuri amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaendelea na haujakamilika.

Kutokana na upelelezi kutokamilika hakimu anayeendesha kesi hiyo Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu, Victoria Nongwa aliutaka upande wa Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi wa kesi hiyo ili iweze kusikilizwa kabla ya kuiahirisha na kuipanga tarehe tajwa hapo juu.

Mkurugenzi huyo wa Jamii Forum anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Kesi hiyo imetajwa kusikilizwa tena Februari 16 mwaka huu baada ya kuhairishwa leo kutokana na upelelezi kutokamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *