Kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imefutwa na mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi.

Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

Mlalamikaji amedai kwamba wakati NHC inamtoa kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia ulikuwepo lakini haukutekelezwa ipasavyo.

Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba walikuwa na mahusiano ya mwenye nyumba na mpangaji, mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya utekelezaji wake.

Naye wakili wa upande wa Mbowe Hotel Ltd, John Mallya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi na kuongeza kuwa wakiipata nakala hiyo wanaweza kuamua iwapo wakate rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *