Mfanyabiashara maarufu na mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupandishwa kizimbani leo.

Manji amefikishwa katika mahama hiyo mapema leo asubuhi akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Manji ambaye alilazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la moyo jana alirudishwa rumande na leo amepandishwa kizimbani kutokana na kosa hilo.

Kwa mujibu wa kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa Manji anakabiliwa na kesi hiyo baada ya kupimwa kwa mkemia mkuu na vipimo vyake vimeonesha kwamba anatumia dawa za kulevya.

Manji ni miongoni mwa watu waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambaye aliripoti kiuo kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Central) na kuwekwa ndani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *