Kesi inayomkabili muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael maarufu ‘Lulu’ imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine mahakamani.

Shahidi huyo aliyetajwa ni Bi. Josephine Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imehairishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Josephine Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *