Kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Kundi la Tip Top Connection, Babu Tale katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeahirishwa mpaka Septemba 12 mwaka huu.

Meneja huyo anakabiriwa na kesi ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake.

Kwa mujibu wa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mustapha Sian amesema sababu kubwa ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kwamba aliyetakiwa kuitolea hukumu ambaye ni Msajili Projest Kahyoza hayupo mahakamani kikazi.

Katika kesi hiyo Babu Tale pamoja na mdogo wake kutoka kundi la Tip Top Connection wanatakiwa kuieleza mahakama kwa nini wasifungwe jela ama kumlipa Shehe Mbonde kiasi cha Sh. Milioni 250 kama fidia ya kusambaza DVD hizo za mawaidha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *