Nchi ya Kenya kwa mara ya kwanza imeanza kuuza magari yanayotumia nishati ya umeme badala ya nishati ya mafuta.

Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo hii ikiwa na maana kwamba hazitoi moshi au gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani kwa hivyo yanafaa mazingira husika.

Vile vile magari hayo yana uwezo wa kusafiri umbali wa takriban kilomita 90 hadi 135 kabla ya betri zake kuisha chaji, kasi yake ya juu zaidi ikiwa kilomita 180 kwa saa.

Kenya 2

Changamoto iliyopo ya magari hayo ni Upungufu wa vituo vya kuchajia na huenda ukakwama ukiwa katika maeneo ya mashambani ambapo hamna nishati ya umeme ama pia vituo vya kuweka chaji.

Kwasasa magari hayo yameanza kutumika maeneo ya jiji la Nairobi kutokana na maeneo mengine kuwa na tatizo la nishati ya umeme.

kenya 3

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *