Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo amezindua reli mpya kati ya mji wa Mombasa hadi Nairobi ikiwa ni miezi 18 baada ya kukamilika.

Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake.

Mradi huo umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa reli ya China kukamilika.

Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha nchi za Sudan Kusini, DR Congo ,Burundi pamoja na mij wa Mombasa nchini Kenya.

Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.

Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.

Rais Uhuru Kenyatta alisema wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ambayo imeanzishwa mwamko mpya katika historia ya Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *