Baada ya Edward Lowassa kusema kuwa atamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya, hatimaye mgonbea wa upinzani Raila Odinga amtaka Lowassa kutofanya hivyo.

Raila Odinga ambaye ni mgombea urais kupitia umoja wa muungano wa upinzani wa NASA amemuomnba Lowassa kumuunga mkono kwenye uchaguzi huo wa Kenya.

Ombi hilo la Odinga linakuja baada ya Edward Lowassa kusema kuwa wakati wa uchaguzi wa Tanzania mwaka 2015, Raila Odinga alikuwa anamuunga mkono Rais Magufuli ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Lowassa.

Odinga amesema kuwa Lowassa pamoja na Rais John Magufuli waliochuana kwenye uchaguzi mkuu uliopita ni marafiki zake, na kuwaomba wote wamuunge mkono kwenye uchaguzi huo.

Lowassa ana ushawishi kwa kiasi fulani kwenye uchaguzi huo kwa kuwa ni kiongozi mkuu wa Wamasai (Leigwanan) katika ukanda wote wa Afrika Mashariki.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo pia kimeweka wazi kuwa kitamuunga mkono Kenyatta kwa kuwa kinaridhika na namna alivyofanya kazi hususan kuruhusu demokrasia nchini kwake.

Kwa upande wa msemaji wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Philip Etale alisema kuwa Odinga ni rafiki wa Lowassa na Magufuli na kwamba asingependa urafiki huo upotee kwa sababu za kisiasa..

Kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi ambao unatajwa kuwa na ushindani mkubwa zaidi kwani katika uchaguzi uliopita, Kenyatta na Odinga walizidiana kwa kiasi kidogo cha kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *