Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch limeituhumu Kenya pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi (UNHCR) kwa kutofuata sheria katika kuwarejesha wakimbizi Somalia.

Shirika hilo kwenye ripoti yake iliyotolewa imesema Kenya haiwapi wakimbizi fursa ya kuamua iwapo wanataka kusalia kambini Dadaab au kurejea Somalia.

Mkurugenzi wa masuala ya haki katika Human Rights Watch Bill Frelick amesema UNHCR haitawapa wakimbizi habari sahihi kuhusu hali halisi ya usalama Somalia.

Serikali za Kenya na Somalia zimesema wakati umefika wa kufunga kambi hizo.

Kenya ilikuwa imetangaza kwamba kambi ya Dadaab itafungwa kufikia mwezi Novemba mwaka huu.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuna baadhi ya wakimbizi ambao wameamua kuondoka kambini wakihofia kuondolewa kwa lazima mwezi Novemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *