Kocha wa timu ya riadha ya Kenya inayoshiriki michuano ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro, John Anzrah amerudishwa nyumbani kwa kosa la udanganyifu.

Mkuu wa timu ya Olimpiki ya Kenya, Kip Keino amesema John Anzrah aliigiza kama miongoni wa wakimbiaji wa mita 800 na kutoa sampuli ya mkojo kwa niaba ya mkimbiaji Ferguson Rotich.

Wakaguzi wa dawa za kusisimua misuli waligundua udanganyifu huo baada ya kuangalia picha za kitambulisho alichokuwa amevaa ndipo walipogundua kuwa sura ya Anzrah haeindani na mchezaji aliyefanya uchunguzi.

Anzrah ni afisa wa pili kutoka kenya kurejeshwa nyumbani wa kwanza akirudishwa kwa kosa la kuomba rushwa ili kukwepa upimaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Baadhi ya wanariadha wa Kenya walishindwa kufuzu vipimo vya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu huku shirika la kupambana na matumizi ya dawa hizo WADA likiiondoa Kenya kwenye nchi zilizoshindwa kutimiza masharti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *