Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Uingereza na mfungaji bora wa timu hiyo Kelly Smith ametangaza kuachana na mchezo huo akiwa na umri wa miaka 38.

Smith aliyekuwa akichezea klabu ya wanawake ya Arsenal alikuwa ndiye kinara wa mabao kwenye timu ya taifa akiwa amepachika wavuni jumla ya mabao.

Wakati wa kuichezea timu ya taifa lake Smith alifanikiwa kuitwa kikosini mara 117 na kushiriki kwenye michuano mikubwa sita na aliiwakilisha Uingereza kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 2012.

Akiwa na kikosi cha Arseanal, Smith alifanikiwa kushinda makombe matano ya FA huku akifunag mabao matano kwenye fainali hizo.

‘Ninajisikia sahihi kuachana na soka kwa sasa. Nafikiri ni muda muafaka kabisa na ninaamini nilikuwa na wakati mzuri kwenye michezo nikiwa na timu ya taifa pamoja na timu ya Arsenal’

Smith ambaye alistaafu soka la kimataifa mwaka 2015 ameshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia mara mbili na michauno ya Ulaya mara nne akifunga bao kwenye fainali ya kombe la Ulaya mwaka 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *