Mwanamuziki nyota wa Marekani, Kelly Rowland anatarajia kutoa kitabu chake cha kwanza na kuandika yote aliyopitia baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Kitabu hiko amekipa jina la ‘Whoa, Baby!:’ kinatarajiwa kutoka mwezi wa tatu mwaka 2017.

Kitabu hiko kinaelezea jinsi mwanamke aliyepta mtoto wake wa kwanza na kupata mshtuko wa jinsi maisha yake yalivyobadilika na hajui cha kufanya ‘Whoa, Baby!:’

Kitabu hiko kimeandikwa na Kelly Rowland mwenyewe huku akipata msaada mkubwa wa daktari Tristan Emily Bickman.

Kelly amesema hakuna mtu alimwambia kitakacho mtokea kwenye mwiliwake, akili na hisia zake baada ya kupata mtoto na alibidi ajifunze mwenyewe ndio maana anaona ni sawa kuwapa wamama elimu hii mapema.

Kelly mwenye umri wa miaka 35 ameandika kitabu hiko kutokana na maisha baada ya kupata mtoto wake wa kwanza ‘Titan Jewell’.

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa waanzilishi wa kundi la Destiny’s Child lilikuwa linaundwa na wasanii wa kike watatu akiwemo Kelly Rowland, Michell William na Beyonce Knowless.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *