Mwanamuziki nyota wa Marekani, Justin Bieber ameondoka jukwaan wakati akitumbuiza kwenye tamasha lake mjini Manchester baada ya mashabiki kupiga kelele wakati anaimba.

Wakati wa tamasha hilo Bieber amesema ‘Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi munayonipa na nathamini ukarimu wenu’.

Mwanamuziki huyo aliendelea kusema ‘Lakini kelele munazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe’.

Mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele Mwanamuziki huyo aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.

Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha lake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *