Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa kwasasa hawezi kuzungumzia uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Anna Mghwira.

Zitto amesema kuwa ‘Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Pia amesema ‘Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.

Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.

Aliyeteuliwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu. Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji kikao cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *