Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesisitiza kuwa mpinzani wa leo Arsenal atafurahi kutokana na kuchezesha kikosi B leo.

Mourinho amesema kuwa “Wengerukweli atanifurahia kwa sababu nitabadilisha timu yangu dhidi ya Arsenal kwani tunapaswa kuwa na ubinadamu na kwa wachezaji.

Tunapaswa kuwa na busara na (kuwatumia) kwa akili katika uhusiano kwa hali yetu ya Premier League.

Kocha huyo amesema kuwa “Mechi yetu ya mwisho dhidi ya Swansea ilikuwa ya mwisho kwetu kupigania nne-bora, hivyo nitapumzisha wachezaji wangu”.

“Hatutakwenda Arsenal kusema “tufungwe tano ama 6-0”. Tunakwenda pale kupigania matokeo.

“Lakini siwezi sasa kuchezesha timu ile ile ambayo ilicheza Hispania na Celta Vigo halafu irudie tena Alhamisi ijayo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *