Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ametoa pole kwa wafanyabiashara walioathirika na janga la moto kwenye soko la Sido mkoani humo.

Makalla pamoja na kutoa pole hizo amewashukuru wananchi na vyombo vya usalama kwa ushirikiano waliouonesha wakati wa kuhudhibiti moto huo usiendelee kueleta madhara makubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Pia mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa serikali kupitia mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati ya kufanya tathmini ya mali zilizoungua pamoja na kuchunguza chanzo cha moto huo kwenye soko hilo.

RC Makala amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo ili iweze kujua chanzo cha moto huo na hasara iliyopatiakana kwenye janga hilo la moto kwenye soko hilo.

Usiku wa kuamkia leo Soko Kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO, lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa jijini Mbeya linateketea kwa moto  na chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *