Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amejikuta akiingia kwenye matatizo na mpenzi wake baada ya kusema kuwa yeye ni mtu anayefumaniwa sana na wasichana kila siku mtaani kwake.

Msechu amedai muda mchache baada ya kauli hiyo kusambaa mke wake alianza kupigiwa simu na watu mbalimbali kitu ambacho kilimfanya achanganyikiwe kutokana na taarifa hizo.

Kauli hiyo ya Msechu ilikuja baada ya kuulizwa kuwa wasichana wengi hawapendi kutoka kimapenzi na wanaume wenye vitambi ndipo muimbaji huyo akajibu mbona yeye mtaani kwake wasichana wengi wanamgombania na anafumaniwa sana mtaani kwake.

Msechu amedai kauli hiyo aliitoa kwa mzaha na baadhi ya watu walishindwa kuielewa na kuanza kumpigia simu mpenzi wake kutokana na kauli hiyo tata ya Peter Msechu.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa “Yaani baada ya ile kauli kusambaa hawakunitafuta mimi wala media, wakatafuta mzazi wangu, nilikwambia mwanao mwambie aache muziki sasa angalia anafumaniwa kila siku. Mke wangu akajazwa maneno ametoka ofisini amedata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *