Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa halikutumia nguvu wakati wakiwatawanya walemavu kwa mabomu ya machozi baada ya kuziba Barabara ya Sokoine wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa.

Hayo yamesemwa na kaimu wa mkuu wa jeshi kanda maaulum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya wakati akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Jeshi hilo limesema kuwa halikutumia nguvu kupita kiasi kama inavyodaiwa lakini walitumia nguvu kulingana na watu waliokuwa wakifanya maandamano hayo.

Kamanda Mkondya amesema kuwa “Ulemavu, nataka nitoe rai kwa wananchi ulemavu sio kibali cha wewe kuvunja sheria wala ulemavu haukupi wewe kibali cha kuvunja sheria za nchi.

Amesema kuwa “Hawa walemavu walifanya makosa, wamevamia Ofisi ya Mkurugenzi  wa Manispaa lakini pamoja na hivyo wakaziba njia.

Mwisho amemaliza kwa kusema “Tumejaribu kuongea nao kuwasihi kwamba wafungue njia lakini pia wateue viongozi wao kwenda kushughulikia matatizo yao lakini walikaidi. Kwa hiyo, ikabidi tutumie nguvu kidogo tukaenda kuwaondosha tukafungua barabara na wananchi wengine wakaendelea na shughuli zao.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *