Mwanamuziki wa Marekani, Katy Perry amekuwa mtu wa kwanza duniani kufikisha wafuasi milioni 100 katika mtandao wa Twitter.

Mtandao huo ulichapisha kanda ya video inayoonyesha jumbe zake zote tangu alipojiunga na mtandao huo pamoja na ujumbe unaosema “Today, we #WITNESS history”{Leo #Tumeshuhudia Historia} Witness ni jina la albamu mpya ya Perry.

Mwimbaji wa Canada Justin Bieber ni wa pili kwa idadi kubwa ya wafuasi katika mtandao wa Twitter akiwa na milioni 96.7 naye rais Obama akiwa wa tatu na wafuasi milioni 91.

Wengine wanaoshirikisha orodha wa watu 100 ni wasanii, wanamichezo, kampuni za habari, na wanasiasa wachache kulingana na mtandao wa Twitter.

Rais wa Marekani Donald Trump ndiye kiongozi anayefuatwa sana aiwa katika nafasi ya 33 baada ya kuwa na wafuasi milini 32.4.

Naye waziri mkuu wa India Narendra Modi akiwa na wafuasi milioni 30.7 kwenye mtandao huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *