Katibu mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji na wabunge wawili wa chama hicho na viongozi wengine  sita wa chama hicho waliokamatwa juzi na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma wameachiwa huru leo.

Hayo yamethibitishwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene leo mara baada ya kuachiwa viongozi hao.

Wenigine ni Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda  Sakuru kwa kile kilichoelezwa kuwa ni maagizo aliyopewa ODC wa Nyasa kuwakamata viongozi hao na kuwaweka selo kwa saa 48.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali, polisi walivamia kikao cha ndani cha Chadema kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Dk. Mashinji ya kukagua shughuli za chama katika kanda hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *