Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Dk Mashinji anakwenda kuripoti kipindi ambacho Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa chama hicho, Kigaila Benson anaendelea kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Akizungumza leo Oktoba 25,2017 mwanasheria wa Chadema, Fredrick Kihwelo amesema, “Katibu Mkuu ametakiwa kuripoti kwa DCI na sasa natoka hapa Central kwa Kigaila nakwenda huko.”

Amesema suala la Kigaila kupata dhamana au kupelekwa mahakamani litajulikana mchana wa leo baada ya kutakiwa kurudi Kituo Kikuu cha Polisi.

Kihwelo alipoulizwa ni nini sababu ya Dk Mashinji kuitwa kwa DCI, amesema itakuwa ni mwendelezo wa mahojiano na Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za uchochezi alipozungumzia hali ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kigaila ambaye ameshafikisha saa 72 akiwa rumande tangu alipojisalimisha kituoni hapo Jumatatu Oktoba 23,2017 na kuhojiwa kwa kutoa lugha za uchochezi katika mkutano na wanahabari Oktoba 12,2017 makao makuu ya Chadema wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *