Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji, Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kusini pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Zubeda Sakuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho, viongozi hao walipelekwa jana kituoni kuhojiwa ambapo Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alitakiwa kueleza kwanini yuko Mbamba Bay na aeleze amekwenda kufanya nini.
Polisi walimkamata Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, Mbunge Mwambe na Mbunge Zubeda baada ya kuvamia kikao cha ndani kilichokuwa kikiendelea mjini hapo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kukagua shughuli za chama katika majimbo ya kanda hiyo iliyoanza jana, ilieleza taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *